Msikie monagangster akizungumzia Vitamin Music ya Belle9 ft Joh makini.
sauti ya Monagangster
Monday, 27 October 2014
Monday, 20 October 2014
Monagangster azungumzia mapishi ya wimbo wa Vitamin Music
Producer wa muziki wa kizazi kipya wa bongo Monagangster asema kuwa Vitamin Music ni moja kati ya nyimbo nzuri ambazo anaendelea kufanya.
Vitamin Music ni kibao kipya town amabacho msanii Belle9 amefanya,akimshirikisha Joh makini.
Monagangster anauzungumzia wimbo huo kati ya mafanikio yanaendelea katika mziki wa kizazi kipya.mbali na hayo Monagangster amesema kuwa Belle9 anazidi kukua kila anapoachia vibao vyake,hivyo amewataka watanzania kupokea mzigo huo (Vtamin Music). Kusikiliza alicho kisema katika hili nenda kwenye link ya Interview hapo juu.
![]() |
Monagangster akiwa studio kwake maeneo ya mwananyamala. |
![]() |
Monaganstaer |
![]() |
Muonekano wa Kava la wimbo wa Vitamini music wa Belle9 ft Joh Makini |
Thursday, 9 October 2014
Wednesday, 1 October 2014
MWANAMUZIKI RAY C AJA KIVINGINE
Mwanamuziki aliyewahi kutikisa anga za muziki wa bongo fleva Tanzania na Nje ya Tanzania Rehema Chalamila maarufu kama RAY C amesema kuwa tangu ametoka katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuamua kufungua kituo chake kwa ajili ya kutibu watu walioathirika na matumizi ya madawa hayo anajionea fahari na kujivunia.
Mbali na kufungua kituo hiko cha kuwasaidia watumizi wa madawa ya kulevya kuacha madawa hayo,Ray C amesema kuwa kufanya hivyo tuu haitoshi,kitu ambacho kimemfanya afungue mgahawa uitwao Ray C Restaurant, ambao utawasaidia vijana waliopata dawa ya kuacha madawa ya kulevya kufanya kazi,hivyo kutopata fursa ya kufikiri kurudi walikotoka.
Ray C ametoa wito kwa serikali kuendeleza juhudi za kuleta dawa za kufanya watumizi wa madawa hayo kuacha kabisa,na kutoa shukrani zake kwa juhudi zilizofanywa hadi sasa.
Msanii Ray C na mwandishi wa Blog hii wakijiandaa kwaajili ya mahojiano.
Subscribe to:
Posts (Atom)