Wednesday, 1 October 2014

MWANAMUZIKI RAY C AJA KIVINGINE


Mwanamuziki aliyewahi kutikisa anga za muziki wa bongo fleva Tanzania na Nje ya Tanzania Rehema Chalamila maarufu kama RAY C amesema kuwa tangu ametoka katika matumizi ya madawa ya kulevya na kuamua kufungua kituo chake kwa ajili ya kutibu watu walioathirika na matumizi ya madawa hayo anajionea fahari na kujivunia.
Mbali na kufungua kituo hiko cha kuwasaidia watumizi wa madawa ya kulevya kuacha madawa hayo,Ray C amesema kuwa kufanya hivyo tuu haitoshi,kitu ambacho kimemfanya afungue mgahawa uitwao Ray C Restaurant, ambao utawasaidia vijana  waliopata dawa ya kuacha madawa ya kulevya kufanya kazi,hivyo kutopata fursa ya kufikiri kurudi walikotoka.
Ray C ametoa wito kwa serikali kuendeleza juhudi za kuleta dawa za kufanya watumizi wa madawa hayo kuacha kabisa,na kutoa shukrani zake kwa juhudi zilizofanywa hadi sasa.
Msanii Ray C na mwandishi wa Blog hii wakijiandaa kwaajili ya mahojiano.

No comments:

Post a Comment